Idara ya wahadhiri tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Majlisi imefanywa kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) chini ya Ataba tukufu.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na ziara ya Imamu Hassan (a.s), kisha likafanywa igizo lenye anuani isemayo (Mjukuu mkubwa baina ya sumu na mshale), igizo hilo limeonyesha dhulma alizofanyiwa Imamu (a.s), na kuhitimishwa kwa qaswida na tenzi za kuomboleza na kumpa pole Imamu wa zama (a.f).
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake husambaza ujumbe wa Ahlulbait (a.s) kwa kutumia njia mbalimbali za audio na video kwenye mitandao yake.