Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi na mabango yanayoashiria huzuni ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Watumishi wa Ataba tukufu wameweka mazingira ya huzuni katika haram ya Ataba tukufu, kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Yamewekwa mabango ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayozunguka sehemu hiyo, imetumika gundi maalum katika uwekaji wa mabango hayo.
Atabatu Abbasiyya imejipanga kuomboleza msiba huo, kwa kuandaa ratiba maalum inayohusisha ufanyaji wa majlisi za kuomboleza, utoaji wa mawaidha sambamba na kukumbusha kazi kubwa aliyofanya Mtume (s.a.w.w) katika kusambaza Uislamu.