Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanatoa rambirambi kwa kifo cha Imamu Askariy (a.s).

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wanatoa rambirambi kwa kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) kupitia Maukibu ya pamoja.

Maukibu imeanza matembezi yake ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kusimama kwa mistari kisha wakaanza kutembea wakielekea kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba tenzi na mashairi ya kuomboleza, yaliyo amsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Maukibu ikahitimisha matembezi yake ndani ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlisi ya kuomboleza, wameshiriki watumishi wa Ataba mbili na kundi kubwa la mazuwaru watukufu.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hufanya matembezi ya kuomboleza katika kila tukio la msiba wa Ahlulbait (a.s) katika kipindi cha mwaka mzima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: