Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeanzisha jiko kwa ajili ya kugawa chakula kila siku kwa wakimbizi wa Lebanon katika nchi ya Siria.
Kiongozi wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya nchini Siria Sayyid Naafii Ni’mah Mussawi amesema “Tumeanzisha jiko kwa ajili ya kugawa milo mitatu kila siku, kwa wakimbizi wa Lebanon nchini Siria kutokana na mashambulizi ya kinyama wanayo fanyiwa watu wa Lebanon”.
Akaongeza kuwa “Ujumbe huo kwa kushirikiana na ofisi ya Marjaa-Dini nchini Siria umeteua sehemu mbili za kuweka majiko katika uwanja wa karibu na haram ya Bibi Zainabu (a.s), sehemu nyingine itakuwa kwa ajili ya kutunzia misaada inayotoka Iraq na kutoa msaada ya kimkakati na vikapu vya chakula kwa familia za wahanga”.
Huduma hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, na maelekezo ya Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ili kupunguza matatizo wanayopitia watu wa Lebanon.








