Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya kimeweka mabango ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Askariy (a.s) ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Vitambaa na mabango yameandaliwa na idara ya ushonaji na kudarizi chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Ataba tukufu.
Makamo rais wa kitengo cha usimamizi wa haram Sayyid Zainul-Aabidina Quraish amesema “Watumishi wa kitengo wametengeneza mabango yanayoashiria furaha na kuelezea utukufu wa Imamu Hassan Askariy (a.s) katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, inayosadifu mwezi kumi Rabiul-Aakhar”.
Akaongeza kuwa “Muonekano wa furaha umewekwa kwenye kuta na milango ya Ataba tukufu” akabainisha kuwa “Watumishi wa kitengo hiki hugawa mauwa na pipi kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kila tukio la furaha”.
Atabatu Abbasiyya hufanya ratiba maalum katika kila tukio linalohusu Maimamu wa Ahlulbait (a.s), likiwemo hili la kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan Askariy (a.s).




