Majmaa-Ilmi imechapisha kitabu kiitwacho (Miongoni mwa watu wa kwanza kuandika tafsiri ya Qur’ani tukufu).

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imechapisha kitabu kiitwacho (Miongoni mwa watu wa kwanza kuandika tafsiri ya Qur’ani tukufu).

Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema “Watafiti wa kituo cha masomo na tafiti za Qur’ani katika Majmaa, wamefanya utafiti katika Qur’ani walioupa jina la (Wanachuoni wetu waliotangulia), wameangazia kazi zilizofanywa na wanachuoni waliotangulia, waliofikisha mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kwa watu, miongoni mwa wanachuoni hao ni swahaba mtukufu Thabiti bun Dinaar, mwenye dua maarufu iitwayo (Dua ya Abi Hamza Thamali) iliyobeba madhumuni ya Qur’ani”.

Akaongeza kuwa “Mwanachuoni huyo alifanya kazi kubwa ya kuandika kitabu cha tafsiri ya Qur’ani, ni miongoni mwa wabokezi wa kwanza katika sekta ya Qur’ani, alipata matatizo mengi kutoka kwa watawala waovu wakati wa uhai wake, kitabu hiki kimeeleza historia yake na nafasi yake katika elimu, hususan kazi kubwa aliyofanya ya kuandika tafsiri, kwani yeye ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuandika tafsiri ya Qur’ani tukufu”.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inaendelea kutoa machapisho tofauti katika sekta ya Qur’ani kwa faida ya umma wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: