Kitengo cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi matukufu na milango katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea na mradi wa mlango wa Ummul-Banina ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Rais wa kitengo Sayyid Nadhim Ghurabi amesema “Kitengo cha kutengeneza madirisha kinafanya miradi mbalimbali, ukiwemo mradi wa mlango wa Ummul-Banina (a.s), uliopo ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao umeshakamilika kwa kiwango kikubwa”.
Akaongeza kuwa “Kazi za mradi huo imepitia hatua mbalimbali, ikiwemo kukata vipande vidogovidogo vilivyopo kwenye mlango na kuvipaka madini ya dhahabu ya kiwango cha 24”.
Akabainisha kuwa “Watumishi wa kitengo wamepiga hatua kubwa katika mradi wa mlango wa Ummul-Banina (a.s), zimebaki hatua chache za kumalizia na kwenda kuufunga sehemu yake”.








