Ofisi ya Marjaa-Dini mkuu inatoa rambirambi kufuatia kuuawa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) nchini Pakistan

Ofisi ya Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, imetoa rambirambi kufuatia kuuawa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Pakistan.

Ifuatayo ni nakala ya tamko:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

(Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)

Ndugu zangu waumini wa mji wa Pajenaar (Alla akupeni utukufu).

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu na baraka zake.

Kwa mara nyingine magaidi wamefanya jinai mbaya, kwa kushambulia msafara uliokua unatoka Pajenaar kwenda Peshawar, jambo lililopelekea kuuawa waumini wengi na wengine kujeruhiwa.

Tunatoa pole kwenu ndugu zetu. Kwa masikitiko makubwa tunaungana pamoja na familia za wahanga, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe subira na uvumilivu, majeruhi awaponye haraka na mashahidi wetu awaweke katika pepo ya daraja la juu.

Hakika hauza ya Najafu na Maraajii wake wanalaani shambulio hilo baya lililolenga waislamu, tunaiomba serikali ya Pakistan ichukue hatua zinazohitajika katika kusaidia wahanga na kupambana na makundi ya kigaidi, izuwie kushambuliwa waumini na makundi ya kigaidi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu adumishe utukufu kwa watu wa Pakistani.

Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: