Kituo cha kibiashara Al-Afaaf kimewapa zawadi baadhi ya mayatima kutoka taasisi ya Nurul-Hussein Alkhairiyya

Kituo cha kibiashara Al-Afaaf chini ya shirika la Nurul-Kafeel katika Atabatu Abbasiyya, kimewapa zawadi baadhi ya mayatima kutoka taasisi ya Nurul-Hussein Alkhairiyya.

Kiongozi wa kituo Sayyid Muhammad Saidi amesema “Kituo cha kibiashara Al-Afaaf kimefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s) na kugawa zawadi kwa baadhi ya mayatima wa taasisi ya Nurul-Hussein Alkhairiyya”.

Akaongeza kuwa “Hafla imehusisha usomaji wa qaswida na tenzi pamoja na kufanya shindano kwa mayatima kisha kugawa zawadi kwa washindi”.

Tukio hili ni sehemu ya kujenga utamaduni kwa mayatima na kuongeza uwelewa wao, Ataba tukufu inajali watu wa tabaka zote katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: