Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, anapokea watu wanaokuja kutoa salam za Idul-Fitri.
Naibu katibu mkuu wa Ataba Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Ataba, marais wa vitengo na viongozi, wameshiriki kupokea wageni na kupeana pongezi za sikukuu hii tukufu.
Ataba imeshuhudia kundi kubwa la viongozi wa mkoa wa Karbala waliokuja kutoa salam za sikukuu ya Idul-Fitri katika mazingira yaliyojaa bashasha na furaha.
Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu arejeshe tukio hili mwakani tukiwa katika amani na salama.
Muheshimiwa katibu mkuu amemuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada zutu, alinde taifa la Iraq na raia wake awatunuku amani na usalama, aidha ameonyesha kufurahishwa sana na wageni waliofika kutoa salam za sikukuu na akawatakia kwa Mwenyezi Mungu awadumishe katika kheri na wema.

























































