Kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Allamah Sayyid Ahmadi Swafi, amehusia kutunza turathi za Karbala na aina zilizo zoeleka katika usomaji wa Qur’ani tukufu na adhana.
Ameyasema hayo alipokutana na waadhini wa Ataba mbili tukufu Sayyid Muhammad Ridhwa Swarafi na Sayyid Liith Ubaidi pamoja na muelekezaji wa mafundisho ya kidini katika Atabatu Husseiniyya Sayyid Muhammad Swadiq Muhammad, amewapa zawadi kutokana na kazi nzuri waliyofanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1446h.
Muheshimiwa akasema kuwa, mji wa Karbala unautambulisho maalum katika usomaji wa adhana na Qur’ani tukufu, inapasa kutunza turahi hiyo, akasisitiza umuhimu wa kuendelea na mahadhi yaliyozoweleka katika jamii.
Akasema ni muhimu wasomaji wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wawe na utofauti kulingana na utukufu mkubwa wa sehemu hiyo takatifu tofauti na sehemu zingine.
Wasomaji wa Qur’ani tukufu wamefurahi kukutana na Muheshimiwa Sayyid Swafi na kusikiliza maelekezo yake pamoja na kupokea pongezi zake kwa kazi waliyofanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, wakasisitiza kuendelea na usomaji wa Qur’ani sehemu mbalimbali hapa Iraq, kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.