Watumishi wa kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kuweka mabango yanayoashiria huzuni katika kujiandaa kupokea mwezi wa Muharam.
Makamo rais wa kitengo hicho Mhandisi Mahadi Mussawi amesema “Watumishi wameanza kuweka mabango yanayoashiria huzuni katika maeneo ya Maqaam ya Imamu wa Zama (a.f), ikiwa ni pamoja na kubadili bendera ya kubba tukufu na kuweka vitambaa vyeusi kwenye minara ya Maqaam”.
Akaongeza kuwa “Kazi imehusisha uwekaji wa mapambo meusi upande wa wanawake, kuandaa sehemu ya kufanyia ibada na kuratibu uingiaji na utokaji ndani ya Maqaam”.
Akaendelea kusema “Kuna mambo mengi yanaandaliwa kwa ajili ya kupokea msimu wa huzuni, utoaji wa huduma mbalimbali, huduma za afya, taratibu za kidini na mengineyo”.















