Watumishi wa shamba boy ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wanasafisha mto wa Hindiyya katika mji wa Karbala baada ya kuisha msimu wa ziara ya Arubaini.
Kiongozi wa shamba boy Sayyid Muhammad Harbi amesema: “Watumishi wameanza kusafisha mto huo baada ya kuisha msimu wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”, akabainisha kuwa “Kazi imefanywa kwa kutumia vifaa vya shamba boy, wameondoa taka ndani ya mto na kuuweka katika muonekano mzuru”.
Akaongeza kuwa “Watumishi huweka mazingira safi chini ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kudumisha usafi wa mji, hususan maeneo ya karibu na vituo vya kupokelea mazuwaru na kuwahudumia”.





