Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu amekagua maendeleo ya elimu katika chuo kikuu cha Al-Ameed na amejadili mkakati wa uboreshaji

Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Didah Mussawi, wamekagua maendeleo ya elimu katika chuo kikuu cha Al-Ameed, kupitia ziara waliyofanya hapo chuoni.

Katika ziara hiyo wamekutana na rais wa chuo Dokta Judat Nuriy Jash’ami, wamejadili maendeleo ya elimu na mkakati wa uboreshaji, sambamba na kuangalia uboreshaji wa mazingira yaendane na mahitaji ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Ziara hiyo ni sehemu ya kusaidia taasisi za kielimu na kuboresha mazingira ya elimu, sambamba na kuandaa walimu wenye uwezo mzuri wa kuhudumia jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: