Kituo cha Shekhe Tusi cha tafiti na uhakiki chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya, kimeipa machapisho yake ya sasa ofisi ya Imamu Alhakiim katika mji wa Najafu.
Kamati husaidia ofisi na taasisi za kielimu kwa kuzipa machapisho yanayohusu turathi, ambayo husaidia wasomaji na watafiti wa turathi za kiislamu na kuimarisha harakati za kielimu.
Kamati inafanya juhudi ya kupanua shughuli zake za kielimu, kwa kusambaza machapisho yake kwenye ofisi na taasisi za kitafiti, kwa lengo la kutunza turathi na kuzisambaza katika taasisi za elimu na utamaduni.


