Kitengo cha utumishi kimeandaa sehemu maalum za kupumzika zuwaru katika mji wa Karbala

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa sehemu maalum za kupumzika zuwaru kwenye eneo la Mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Jambo hilo ni sehemu ya huduma ya kuandaa mazingira mazuri kwa zuwaru, ikiwemo: kutandika mazulia kwenye eneo la mlango wa Qibla ya malalo takatifu katika usiku wa Ijumaa.

Kitengo kinalenga kutoa huduma bora kwa zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuweka mazingira muwafaka kwao, hususan katika usiku wa Ijumaa ambao hushuhudia idadi kubwa ya zuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: