Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wamefanya usafi katika maeneo yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kazi hiyo ni sehemu ya jitihada za kitengo za kudumisha usafi, na kuweka mazingira bora ya kupokea zuwaru.
Kufanya usafi ni sehemu ya mkakati maalum wa kitengo, na kuhakikisha zuwaru wanapewa huduma nzuri katika mazingira bora yanayowawezesha kufanya ziara kwa amani na utulivu.






