Majina ya washindi kumi yatatangazwa kupitia majukwaa ya Atabatu Abbasiyya siku ya Ijumaa (17/04/2026m) sawa na (28/Shawwal/ 1447h).
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa ahudhurie hafla ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Bibi Fatuma Maasuma (a.s), itakayofanywa siku ya Jumapili (19/04/2026m) sawa na (1/Dhulqadah/1447h), saa 2:30 jioni katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria, atatakiwa kufika katika ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya katika muda usiozidi wiki mbili kuanzia siku ya kutangazwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria) kwa ajili ya kuchukua zawadi yake.
