Kiongozi wa idara hiyo, Bibi Bushra Alkinani amesema: “Kikao kimehudhuriwa na wawakilishi kutoka shule 16 kwenye mikoa tofauti, wamejadili utungaji wa maswali ya mitihani ya mwisho wa mwaka wa masomo itakayofanywa na wanafunzi elfu tatu”.
Akaongeza kuwa “Kamati imetoa maelekezo maalum ya utunzi wa maswali ya mitihani, miongoni mwa maelekezo hayo ni: kuzingatia mpangilio wa ugumu wa maswali, kuweka tatuzi za mifano, kukadiria muda unaofaa wa kujibu swali na kutoa alama kwa uadilifu”, akasema kuwa “Mitihani inahusisha masomo ya msingi manne, ambayo ni: Fiqhi, Aqida, Nahau na Mantik”.
Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya shule za Alkafeel za kidini tawi la wanawake na kuhakikisha inafanywa katika mazingira mazuri yanayoendana na viwango vya wanafunzi kielimu.






