Majlisi imefanywa ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa malalo takatifu na kundi la zuwaru.
Mhadhiri wa majlisi ameongea kuhusu historia ya maisha ya Imamu Swadiq (a.s) na matukio muhimu katika uhai wake, akahitimisha kwa kusoma tenzi.
Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yanayohusu Maimamu watakasifu (a.s) kwa kufanya majlisi na harakati zingine za kitamaduni, kwa lengo la kujenga uelewa wa Dini na kuimarisha misingi ya uislamu.





