Muheshimiwa Sayyid Swafi ameangalia mwenendo wa kazi katika mradi wa shule za Al-Ameed barabara ya Najafu

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ametembelea shule mpya za Al-Ameed, zilizopo barabara ya Najafu kuangalia utendaji wa kazi na kiwango cha ukamilifu.

Muheshimiwa amefuatana na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Ataba tukufu, Mhandisi Dhiyaau Swaaigh, ambae ametoa maelezo kuhusu maendeleo ya mradi huo unaojumuisha shule zilizosanifiwa kisasa zaidi, zitakuwa na mfumo bora wa kimasomo.

Muheshimiwa ameangalia kazi zinazoendelea na kiwango cha ukamilifu wa mradi huo, utakao saidia sekta ya elimu hapa nchini.

Sayyid Swafi amesisitiza umuhimu wa kuwa na majengo ya kisasa ya shule, ili kuandaa mazingira bora ya elimu yanayokidhi mahitaji ya mwanafunzi na kuendana na maendeleo ya kisasa katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: