Kupitia maukibu ya utoaji wa huduma.. idara ya Masayyid imetoa huduma mbalimbali kwa zuwaru katika kumbukizi ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s)

Idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya imetoa huduma mbalimbali kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Sayyid Hussein Aalu Dhiyaau-Dini amesema: “Wahudumu wa idara wanafanya kazi mbalimbali katika kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), ikiwa ni pamoja na kufanya maukibu ya kutoa huduma, inagawa maji baridi na yamoto kwa waombolezaji”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo ni sehemu ya harakati za idara, kutoa huduma bora kwa zuwaru katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: