Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa sehemu za kupumzika zuwaru, katika eneo la mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Wamefanya shughuli mbalimbali zinazolenga kuandaa mazingira bora kwa zuwaru, ikiwemo kutandika miswala milangoni na kwenye viwanja vinavyozunguka malalo takatifu.
Kitengo kinalenga kutoa huduma nzuri kwa zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuandaa mazingira muwafaka hususan katika usiku wa Ijumaa ambao hushuhudia idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara.



