Makamo rais wa kitengo Sayyid Hassan Hashim amesema: “Kitengo kinagawa chakula kila siku, sawa katika siku za kawaida au siku za ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, ugawaji wa chakula ni sehemu ya huduma wanazopewa watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Akaongeza kuwa “Usiku wa Ijumaa umepokea watu wengi wanaokuja kufanya ziara katika mji mtukufu wa Karbala, wahudumu wetu wamegawa sahani elfu 8 za chakula pamoja na kutoa huduma zingine za lazima kwa zuwaru”.
Akafafanua kuwa “Kitengo kinafanya kila kiwezalo katika kuhakikisha kinatoa huduma bora kwa zuwaru wa Atabatu Abbasiyya tukufu, sawa iwe katika siku hizi au wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu”.



