Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeandaa safari ya mapumziko kwa zaidi ya wanafunzi 100 wa mradi wa (Vijana wetu wasomaji) kwenda katika vitalu vya Alkafeel.
Mwalimu wa mradi huo Sayyid Mustwafa Abdulkarim amesema: “Maahadi ya Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya chini ya Majmaa imeandaa safari ya mapumziko kwa wanafunzi wa mradi wa (Kijana wetu msomaji) katika vitalu vya Alkafeel vilivyo chini ya Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa, idadi ya washiriki ni zaidi ya wanafunzi 100, wakiwa na walimu wao, wamefurahishwa na uzuri wa eneo na ubora wahuduma walizopewa.
Makamo kiongozi mkuu wa vitalu Mhandisi Ali Hamza, amesema kuwa wamepokea ugeni wa wanafunzi, na kuwaandalia matembezi maalum ndani ya vitalu hivyo, aidha wamewaelezea aina ya mimea na mauwa yaliyopo ndani ya vitalu hivyo.










