Majmaa-Ilmi imetoa muhadhara wa kielimu kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu katika mji wa Karbala

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetoa muhadhara wa kimalezi kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mji wa Karbala.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Karbala Shekhe Jawadi Nasrawi amesema: “Maahadi imetoa muhadhara wa kimalezi kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mihadhara ya kielimu na kimalezi inayotolewa na Maahadi kwa wanafunzi”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umetolewa katika ofisi za Maahadi, umehudhuriwa na kiongozi wa idara ya tahfiidh katika Maahadi Shekhe Ali Rawiiy, amebainisha nafasi ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) wakati wa uhai wake na namna alivyojenga madrastu Jaafariyya”.

Akafafanua kuwa “Lengo la kutoa mihadhara hii ni kuimarisha utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu kila siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: