Jumuiya ya Al-Ameed imechapisha kitabu cha nane katika mfululizo wa Kunuzul-Aali

Jumuiya ya Al-Ameed imechapisha kitabu cha nane katika mtululizo wa Kunuzul-Aali.

Rais wa kitengo cha maandiko na maoni katika jumuiya Dokta Ahmadi Kaabi amesema: “Kitabu cha msimu wa athari katika khutuba ya Hajaaji inayohusu As-habul-kisaa (a.s) kimeandikwa na Dokta Marwah Muhammad Kaadhim, katika sehemu ya kwanza kimeandika athari ya mwenendo wa Maqami katika nakili za Ahlulbait (a.s) kwenye Hadithul-Kisaa”.

Akaongeza kuwa “Sehemu ya pili ya kitabu hicho imeandika athari za mwenendo wa maqami katika kupanga vipaumbele, na sehemu ya tatu imeandika athari za mwenendo wa maqami katika kutoa hoja ndani ya dalili”.

Akaeleza kuwa “Mfululizo wa Kunuzul-Aali ni sawa na dirisha la maarifa ya elimu za kisekula, linaloimarisha uelewa wa kitamaduni na kielimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: