Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na semina za kuwajengea uwezo wahadhiri wa Mimbari-Husseiniyya.
Wiki hii imeshuhudia somo la tafsiri ya surat Fat-ha, kisha usomaji wa mahadhi ya huzuni katika mada za maombolezo ya Husseiniyya.
Semina hizi zinalenga kuandaa wahadhiri wa Mimbari-Husseiniyya, kwa ajili ya kujiandaa na mwezi wa Muharam na Safar.




