Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimefanya majlisi ya kuomboleza misiba ya Ahlulbait (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala.
Majlisi imehudhuriwa na kundi kubwa la watumishi wa Ataba na zuwaru.
Imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata muhadhara wa kidini uliotolewa na Shekhe Abdullah Dujaili, ameongea kuhusu changamoto na mitihani waliyopitia Ahlulbait (a.s) na umuhimu wa kushikamana nao na kufuata mwenendo wao mtukufu.
Kitengo cha mahusiano hufanya majlisi za kuomboleza misiba waliyopata Ahlulbait (a.s), kusambaza elimu, utukufu wao na kusisitiza kufuata mwenendo wao mtukufu.







