Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amempokea mkuu wa idara ya malezi wa mkoa wa Karbala Sayyid Wamidhu Tamimi.
Kikao chao kumejikita katika kujadili ushirikiano baina ya idara ya malezi ya mkoa na shule za Al-Ameed zilizochini ya Ataba tukufu, na kuboresha mazingira ya malezi katika mkoa.
Wamesisitiza umuhimu wa kushirikiana kati ya taasisi za serikali na zile zilizo chini ya Ataba tukufu, kwa ajili ya kubadilishana uzowefu katika maswala ya kiutawala na kimalezi, sambamba na kufuata mbinu za kisasa katika kuboresha sekta ya elimu.


