Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, Kimesambaza barafu kwenye vituo vya maji vinavyo zunguka Ataba tukufu, ili kuhakikisha upatikanaji wa maji baridi ya kunywa kwa zuwaru.
Kitengo hugawa barafu zinazotokana na kiwanda chake, kwa lengo la kupoza maji kwenye vituo vilivyopo katika barabara ya Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati maalum ulioandaliwa na Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kuweka kazingira mazuri kwa zuwaru na kuwapa huduma bora.




