Mhadhiri wa kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo, Sayyid Hashim Maksusi amesema: Kituo kimeandaa mihadhara ya kitamaduni na kidini katika somo la Fiqhi na Aqida, walengwa ni wanafunzi waliofanya vizuri katika mkoa wa Dhiqaar kwenye shule za msingi na sekondari.
Akaongeza kuwa mihadhara hiyo ni sehemu ya program ya mwanafunzi hodari, inalenga kujenga uelewa wa kidini kwa vijana na kuimarisha moyo wa uajibikaji na utekelezaji wa mafundisho ya Dini tukufu ya kiislamu.




