Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza ushiriki wa askari wake elfu moja katika kulinda misafara ya mahujaji watakaotumia usafiri wa nchikavu

Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kushiriki katika kulinda misafara ya mahujaji watakao tumia usafiri wa nchikavu (barabara).

Kikosi kimesema kuwa, kimeimarisha ulinzi magharibi ya mkoa wa Karbala kwa kuweka karibu askari elfu moja watakao hakikisha usalama wa wageni wa Mwenyezi Mungu kwa kushirikiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama.

Akaongeza kuwa, mkakati wa ulinzi unafanywa kwa kuweka vikosi vya askari katika vituo muhimu, kuanzia Habaria, njia panda ya Nakhibu upande wa Ramadi na Ratwaba, kuweka vituo katika jangwa la Anbaar, kufunga mitambo ya ulinzi na kuweka wanajeshi katika utayali wa kupambana na tishio lolote.

Kikosi cha Abbasi (a.s) hushiriki kila mwaka katika kulinda misafara ya mahujaji wanaotumia usafiri wa nchikavu (barabara) kwa kushirikiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama, jambo ambalo linasaidia wageni wa Mwenyezi Mungu kwenda na kurudi salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: