Katika usiku wa Ijumaa.. kitengo cha utumishi kimeandaa sehemu za kupumzika zuwaru kwa kutandika zulia

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa sehemu maalum za kupumzika zuwaru kwa kutandika zulia maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Jambo hilo hufanywa katika maandalizi maalum ya siku ya Ijumaa, hutandikwa mazulia katika maneneo ya karibu na haram tukufu, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya zuwaru katika siku za Ijumaa.

Jambo hilo ni sehemu ya mkakati wa kitengo cha utumishi, unaolenga kuweka mazingira mazuri kwa zuwaru, yanayo saidia kufanya ibada ya ziara kwa utulivu na kuhakikisha hakuna msongamano unaotatiza zuwaru katika eneo linalozunguka Ataba takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: