Zuwaru wanaendelea kuwasiri katika ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel

Ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya umeshuhudia kuwasiri kwa makundi ya zuwaru wanaokuja kuangalia mali-kale na makumbusho.

Rais wa kitengo cha makumbusho Sayyid Naafii Mussawi amesema: “Kuendelea kuwasiri makundi ya watu katika ukumbi wa makumbusho ya Alkafeel, kunaonyesha ukuaji wa uelewa wa mambo ya kitamaduni kwa zuwaru na hamu ya kufahamu turathi zilizopo katika makumbusho, ukizingatia kuwa wahudumu wa makumbusho hutoa maelezo toshelevu kuhusu mali-kale zilizopo ndani ya makumbusho”.

Zuwaru humiminika kwa wingi kwenye ukumbi wa makumbusho katika siku za Ijumaa, ambazo huwa na zuwaru wengi zaidi, huja kuangalia mali-kale zilizopo katika makumbusho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: