Majmaa-Ilmi imefanya program ya kuhifadhi maneno ya Nahaju-Balagha na kuyafahamu katika mkuo wa Muthanna

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya program ya kuhifadhi maneno ya Nahaju-Balagha na kuyafahamu katika mkoa wa Muthanna.

Program imeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Muthanna chini ya Majmaa, kwa ushiriki wa vikundi viwili, kikundi cha wakubwa wanaoendelea na masomo na kikundi cha vijana wadogo.

Program imehusisha masomo ya kielimu kutoka kwa Shekhe Hani Rabii, amefundisha maneno ya hekima kutoka kwa kiongozi wa waumini (a.s) yanayokomaza fikra na yenye ufasaha mkubwa.

Program inalenga kuhifadhi maneno matukufu na kutambua kwa kina madhumuni yake, hususan kwa wanafunzi vijana, yanasaidia kuwakomaza kifikra na kiroho sambamba na kuwajenga kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: