Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimeandaa gari 20 zinazotumia umeme kwa ajili ya kubeba zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa gari 20 zinazotumia umeme kwa ajili ya kubeba zuwaru wanaoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo Sayyid Husaam Hamdani amesema “Hatua hiyo inatokana na msongamano wa watu katika mji kutukufu wa Karbala”. Akasema kuwa “Gari hizo zinasaidia kupunguza msongamano wa zuwaru na kurahisisha ufanyaji wa ziara hususan kwa wazee na watu wenye ulemavu”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa gari 20 zinazotumia umeme ambazo ni rafiki kwa mazingira, gari hizo zimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayoendana na mazingira ya mji wa Karbala unaoshuhudia msongamano mkubwa wa zuwaru”.

Akabainisha kuwa “Jambo hilo ni sehemu ya mradi endelevu wa kuhudumia zuwaru, sambamba na kuenyesha namna Atabatu Abbasiyya inavyo jali na kuthamini zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: