Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Makamo rais wa kitengo Shekhe Aadil Wakili amesema “Hakika semina hizi zinasaidia kujenga uelewa wa hukumu za kiislamu kwa watumishi, hususan mambo yanayohusisna na udhu, kuoga na kutayamam, semina imepewa jina la (Semina ya Imamu Sajjaad –a.s-)”.
Akaongeza kuwa, semina itadumu kwa muda wa siku kumi, kila siku kutakuwa na masomo matatu, kwa ushiriki wa zaidi ya watumishi 150 kutoka vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Akasisitiza kuwa kitengo cha Dini kinaendelea na semina hizi, hadi ziwafikie watumishi wote wa Ataba tukufu.



