Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefanya semina inayohusu uandishi wa tafiti za kielimu

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina kuhusu mfumo wa uandishi wa tafiti kitaalamu.

Mkuu wa maahadi Bibi Manara Aljaburi amesema: Semina imehusisha watumishi wa Al-Ameed, wamefundishwa mambo ya msingi katika uandishi wa tafiti, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa anuani, masharti ya kielimu yanayohitajika kwa mtafiti sambamba na kutambulisha mifumo ya utafiti wa kielimu.

Akafafanua kuwa semina hizi zinalenga kukuza taaluma na kuboresha mwenendo wa elimu.

Semina hii ni sehemu ya program endelevu inayofanywa na Maahadi, inalenga kuboresha vipaji vya watumishi katika sekta mbalimbali kupitia mifumo mbalimbali ya kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: