Kwa mnasaba wa Idul-Ghadiir.. Idara ya Masayyid imetoa huduma mbalimbali kwa zuwaru

Watumishi wa idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya wametoa huduma mbalimbali kwa zuwaru kupitia maukibu kwa mnasaba wa Idul-Ghadiir.

Wametoa huduma kupitia maukibu iliyopo katika barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni ugawaji wa vinywaji baridi na chakula kwa zuwaru wanaokuja kuadhimisha siku hii tukufu.

Watumishi wa idara ya Masayyid hutoa huduma mbalimbali katika siku za kuadhimisha matukio ya kidini na siku za Ijumaa, kama sehemu ya ratiba yake ya utoaji wa huduma bora kwa zuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: