Mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria.. Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umeshiriki katika kushindikiza muili wa Marjaa-Dini Shekhe Fayaadh katika mji wa Najafu

Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya umeshiriki katika ushindikizaji wa muili ya Marjaa-Dini Shekhe Muhammad Is-haqa Alfayaadh (r.a) katika mji wa Najafu.

Ameshiriki pia kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba Alamah Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya viongozi wa Ataba na wahudumu, pamoja na kundi kubwa la walimu wa Hauza, wanafunzi, viongozi wa Dini, viongozi wa kijamii na kundi kubwa la waumini.

Waombolezaji wametaja athari kubwa iliyoachwa na mwalimu huyo wa Hauza katika mji wa Najafu, umri wake wote ameutumia katika kutumikia Dini na kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s).

Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani ametoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Marjaa-Dini Ayatullah Shekhe Muhammad Is-haqa Alfayaadh (r.a), amepongeza mwenendo wake kielimu na mchango mkubwa aliotoa katika Hauza, na kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: