Kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho.. watu wa Karbala wanafanya majlisi ya kuomboleza sambamba na kukaribia kwa mwezi wa Muharam

Watu wa Karbala kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba tukufu, wamefanya majlisi ya kuomboleza kama sehemu ya kujiandaa na kuupokea mwezi wa Muharam.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Kadhim Swalehe Mahadi amesema: “Majlisi ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka ambao hufanywa na watu wa Karbala kujiandaa na maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein (a.s)”, akabainisha kuwa “Majlisi imehudhuriwa na wawakilishi wa Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya”.

Kiongozi wa maukibu ya Baabu Haani Sayyid Abdu-Ali Abdulkhaliq Al-Hamiri amsema, “Mawakibu za Karbala zimepewa zawadi kutoka kitengo cha Maadhimisho, kutokana na kazi kubwa zinazofanya ya kuhudumia zuwaru na kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya”.

Akaongeza kuwa “Zawadi hizo zinalenga kupongeza na kushajihisha huduma bora zinazotolewa na wahudumu wa Husseiniyya, sambamba na kazi nzuri inayosaidia kurahisisha maombolezo ya miezi ya huzuni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: