Majlisi imefanywa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Shekhe Abdulmahadi Karbalai na Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya viongozi wa Ataba mbili tukufu, viongozi wa kidini, kijamii na kundi kubwa la waumini na wanafunzi wa kidini.
Wahudhuriaji wametoa salam za rambirambi kwa ndugu zake na wapenzi wake, aidha wamemuomba Mwenyezi Mungu amrehemu na kumuweka mahala pema peponi na aipe subira na utulivu familia yake.
Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani alitoa salam za rambirambi kufuatia kifo cha Marjaa-Dini Ayatullah Shekhe Muhammad Is-haqa Alfayaadh (r.a), akapongeza safari yake kielimu na huduma kubwa aliyotoa katika kutumikia hauza na kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s).
















