Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) kimekamilisha maandalizi ya mwezi wa Muharam

Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha maandalizi ya kupokea mwezi wa Muharam, kimeweka mazingira mazuri kwa zuwaru na waombolezaji.

Rais wa kitengo Sayyid Adnani Dhaifu amesema: “Kitengo kimekamilisha maandalizi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Muharam, tumeweka mazingira mazuri ya kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya”.

Akaongeza kuwa: “Maandalizi yamehusisha uwekaji wa mabango meusi yanayoashiria huzuni, baadhi ya maeneo yamefunikwa kitambaa cha Sarani, aidha tumefunga kituo kipya cha umeme, tumejipanga kutoa huduma bora kwa zuwaru”.

Maandalizi haya ni sehemu ya mkakati maalum wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wa kuhuisha matukio na ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu katika mwezi wa Muharam na Safar, kwa kutoa huduma bora kwa zuwaru na kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: