Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesisitiza kuwa kazi ya tablighi ni jukumu la wote na ina athari kubwa katika kujenga jamii.
Ameyasema hayo alipokutana na katibu mkuu wa Majmaa-Ahlulbait (a.s) Muheshimiwa Shekhe Ridhwa Ramadhani na ugeni aliofuatana nao, wameongea kuhusu mambo ya kitamaduni na kitablighi, na namna ya kushirikiana baina ya taasisi mbili, kwa njia ambayo itasaidia katika kuhudumia uislamu halisi.
Akaongea kuhusu umuhimu wa kusoma mazingira ya sasa na kubaini changamoto zilizopo katika jamii za wafuasi wa madhehebu ya Shia na uzowefu wake kihistoria, kwa kuangalia yaliyojiri kwa kiongozi wa waumini na Bibi Zaharaa (a.s), mafundisho yanayopatikana kutokana na changamoto walizo pitia na namna ya kunufaika na mafungisho hayo katika kupambana na changamoto za sasa.
Akausia kunufaika na vikao hivi kwa kuandaa program za kitamaduni na kimaadili zinazolenga tabaka la vijana, hususan wanafunzi wa vyuo, sambamba na kunufaika na matukio mbalimbali, zikiwemo hafla za kuhitimu chuo, kiapo cha Utii ndani ya haram ya Imamu Ridhwa (a.s), mambo ambayo huacha athari kubwa katika nyoyo za wahitimu, na huchangia katika kupambana na changamoto za kifikra na kitamaduni.
Akasisitiza kuwa mkakati wa Imamu Hussein (a.s) ulikuwa na utaendelea kuwa fundisho lenye athari kubwa kihistoria, lenye matokeo chanya na lililofelisha njama za adui, akasisitiza umuhimu wa kazi ya tablighi inatakiwa kufanywa na kila mtu kwa nafasi yake, na jambo hilo lina athari kubwa katika kujenga jamii.

