Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kikao cha kujadili maandalizi ya mwezi mtukufu wa Muharam.
Kikao hicho kimeongozwa na rais wa kitengo Shekhe Ali Mujaan Rabii, mbele ya makamo wake na viongozi wa idara, wamejadili mkakati maalum katika mwezi wa Muharam.
Amesema kuwa: “Kitengo kilianza mapema kufanya maandalizi ya mwezi mtukufu wa Muharam, jambo la kwanza kilifanya mkutamo maalum wa kujadili mkakati wa mwezi wa huzuni na ratiba za harakati za kidini na kitablighi”.
Akaongeza kuwa “Kikao kimejikita katika kujadili maandalizi ya kitengo na kuhimiza wahudumu wafanye kazi kwa bidii katika kuhudumia zuwaru na kuweka mazingira mazuri ya kuhuisha matukio ya Husseiniyya wakati wa mwezi wa Muharam”.
Akafafanua kuwa “Kitengo kinajali uboreshaji wa huduma za kitablighi kwa watu wanaokuja kufanya ziara”.


