Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amefanya ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) muda mchache kabla ya kubadili bendera ya kubba la malalo yake takatifu.
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya Jumanne, yameshuhudia shughuli ya kubadilisha bendera ya kubba lake takatifu, bendera nyekundu imeshushwa na kupandishwa nyeusi, kama ishara ya kuingia mwezi mtukufu wa Muharam mwaka 1448h.
Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia idadi kubwa ya zuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, wamekuja kushiriki katika shughuli za kubadilisha bendera mbili na kuhuisha usiku wa kwanza katika mwezi mtukufu wa Muharam.









