Atabatu Abbasiyya tukufu, imeomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), kupitia majlisi ya kuomboleza ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya majlisi kila siku mara tatu (Asubuhi, mchana na jioni) kwa muda wa siku kumi, kutokana na ratiba ya mwezi mtukufu wa Muharam.
Majlisi imehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami, baadhi ya marais wa vitengo, watumishi wa Ataba na kundi kubwa la zuwaru.
Mhadhiri wa majlisi alikuwa ni Sayyid Hashim Albatwatwa, ameeleza tukio la Twafu na yaliyojiri kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika mazingira yaliyojaa huzuni.
Majlisi hiyo ni sehemu ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) wa kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya haram tukufu, kwa lengo la kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).




