Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameandaa milango ya haram tukufu kwa ajili ya kupokea mawakibu Husseiniyya

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameandaa milango ya haram tukufu kwa ajili ya kupokea mawakibu Husseiniyya

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameandaa milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya mawakibu Husseiniyya zinazokuja kuomboleza katika mwezi wa Muharam.

Watumishi wa kitengo cha kulinda nidham katika Ataba tukufu kwa kushirikiana na kitengo cha kusimamia haram tukufu, wametandika mazulia kwenye milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuongoza matembezi ya mawakibu Husseiniyya, zuwaru na matembezi ya Towareji.

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinafanya kila viwezalo katika kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa zuwaru wanaokuja Karbala kufanya maombolezo ya Ashura mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq.

Atabatu Abbasiyya imeweka mkakati maalum wa kuhudumia mawakibu Husseiniyya wakati wa mwezi wa Muharam, kwa namna ambayo inaendena na matembezi ya ndani ya haram tukufu na maeneo yanayozunguka sehemu hiyo, na kuweka mazingira mazuri kwa waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: