Atabatu Abbasiyya inaendelea na majlisi za kuomboleza kwa siku ya tatu ndani ya haram tukufu

Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kufanya majlisi ndani ya Haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa siku ya tatu katika mwezi wa Muharam.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imeandaa majlisi zinazohudhuriwa na idadi kubwa ya zuwaru na waombolezaji.

Mhadhiri wa majlisi alikuwa ni Shekhe Ali Mujaan, ameeleza umuhimu wa kuhuisha muhanga wa Imamu Hussein (a.s) kwa kueleza yaliyojiri kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) siku ya Ashura.

Majlisi imepambwa na usomaji wa qaswida na tenzi za uombolezaji kutoka kwa muimbaji wa Husseiniyya Hamidi Tamimi, katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi.

Majlisi hizo ni sehemu ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), wa kufanya majlisi za uombolezaji ndani ya haram tukufu, majlisi hufaywa saa 12 asubuhi, saa 7 Adhuhuri na saa 2 usiku ndani ya haram tukufu, kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi katika mwezi wa Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: